USHINDANI WALA SIO UFISADI NDIYO TISHIO KUBWA KWA MAENEDLEO YETU

Posted on

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na malalamishi kutoka raia na viongozi mbali mbali humu nchini Kenya wakilalamikia ongezeko kubwa mno la ripoti za ufisadi toka sekta mbali mbali za serikali yetu tukufu. Tumepata habari nyingi za kashfa tofauti ambazo zime tuwekea wananchi mizigo mizito mno ya madeni. Wengi wetu wame tabiri miaka ijayo yenye kuhitaji uvumilivu na ukakamavu maana tunaweza kuwa na wakati mgumu.

Tumelaumu ufisadi sana kwa kutupotezea fedha nyingi na kumrudisha nyuma mwananchi wa kawaida na kumuingiza kwenye limbwi la umasikini ambalo lita athiri sana vizazi vijavyo. Hebu tafakari hili ndugu yangu; mtu anapoishi katika kitongoji duni cha kutawaliwa na ufukara na dhiki maisha yake na ya vizazi vyake yanaweza kuathirika milele! Katika mazingara hayo ni vigumu upate shule nzuri zenye kuwapatia watu elimu bora maana hakuna pesa za kuwalipa walimu wazuri waliofaulu kwa kiwango cha juu kwenye taaluma yao na kwa hiyo shule hizo huambulia kuajiri walimu ambao stakabadhi nzao ni za kiwango cha chini kidogo kwa maana hao ndiyo watakubali kulipwa mishara duni.

Sasa tukiwa na waalimu duni katika vitongoji duni vya ufukara, sio jambo la ajabu kwamba suhemu hizo elimu itakuwa ya chini ukilinganisha na sehemu zingine. Hilo litahakikisha kwamba kiwango kikubwa mno cha watoto wanaopitia shule hizo watakosa kuendeleza masomo yao ya msingi na kuingia shule za upili. Wanaofulu kuendelea pia hujipata kurudi kwenye mazingara yale yale kutokana na ukosefu wa fedha za kuwapeleka kwenye shule zenye hadhi ya juu na elimu bora zaidi. Sasa basi, watu hao wanapo maliza shule ya upili, huwa mara nyingi wanakosa kuendeleza masomo na kujipata kurudi kwenye vitongoji duni hivyo kuendeleza umaskini. Mtu mwenye elimu duni hupata kazi duni ambayo mara nyingi ni kazi ya mikono. Akiwa na kazi yake duni atarudi kuishi kitongoji duni ambako ataoa ama kuolewa na mtu duni na kwa hiyo maisha yao yatarudia ya wazazi wao. Nao pia wakibarikiwa watoto, wale waototo watapelekwa shule duni humo vtongojini wanamoishi, kwa hiyo inakuwa ni mzungukuo wa ufukara katika vizazi vyao. Hilo ni jambo la kuniskikitisha mimi mno!

Huu ni ukweli wa mambo kwa raia, na watu wote watakubaliana na mimi ya kwamba athari zote hizo zinasababishwa na ufisadi. Nauliza watu leo hii….JE NA UFISAFDI UNASABABISHWA NA NINI????. Huwezi kumaliza ufisadi bila kukata mizizi inayofanya matunda ya ufisadi kunawiri! Ama? Sindio! Ufisadi kama athari zozote zile kwenye jamiii ipo na mizizi, na mizizi ya ufisadi ni USHINDANI KATIKA JAMII.

Ushindani ni jambo ambalo limetundikwa ndani ya nafsi zetu, fikra zetu, mawazo yetu na maisha yetu. Ushindani tumefundishwa kwa ustadi kupitia elimu ya shule zetu na hata kupitia malezi ya familia. Utapata wazazi wanapendelea mtoto flani kushinda wengine maana huongoza shuleni. Shuleni nako pia utapata mtu anayeshinda wengine darasani anaonekana mwenye akili na mwenye haki ya kuonyeshwa mapenzi zaidi kuliko wale wanao shindwa kufikia kiwango flani. Tayari tunatuma ujumbe kwa wale wanao kosa kufaulu zaidi ya kwamba hawastahili mapenzi, uaminiifu au nafasi za uongozi flani kwenye nyumba na hata pia shuleni. Kwa mfano ni jambo gumu sana upate “Headboy” ama “Headgirl” ambaye darasani huwa anavuta mkia ki matokeo ya mitihani. Hapo ndiyo tunapo fanya roho ya ushindani kushika mizizi na kunawiri maishani mwetu. Linaonekana kuwa jambo la kawaida maishani maana wazazi wanalikubali na kuliendeleza na waalimu nao wana linyunyizia nafaka mashuleni. Basi jamii inakuwa yenye ushindani ili mtu akubalike! Shuleni tunaambiwa kuwa ushirikiano ni hatia, haswa kwa “assignments” tunazopewa.

Tunashindana katika kila jambo. Roho hiyo hufanya watu wengine wasikubali wenzao washinde pia maishani. Watu hao huona sio vyema sote tufaulu maana hao hawatawekwa katika hadhi ya juu nay a sifa na kwa hiyo wanafanya yote wanayoweza kuweka wenzao kavtika limbwi la ufukara na umasikini ndiyo watu wale wabaki kuwa watumishi wao na vizazi vyao kuwa watumishi wa watoto na wajukuu wao nao. Wametaka wabaki washindi milele na mshindi hawezi kupatikana hadi kuwe na mshindwa! Watafanya kila namna ili mradi wengine wabaki washindwa maishani mwao. Jambo hili ndilo hupelekea wengine kuamulia kuwa wafisadi maana hawataki waonekane washindwa katika jamii. Watafanya kila namna wawe washindwa na waonekane watu wenye hadhi ya juu katika jamii.

Tunashindana shuleni, tunashindana majirani, tunashindania mapenzi ya wazazi majumbani, tunashindania sifa kwa wasanii na kunyima wengine nafasi haswa wenye uwezo wa kufaulu zaidi ki talanta ili wabaki chini na kuchagua tunao hisi hawatupatii ushindani mkubwa kwenye sifa maana tuta wakulia. Vyombo vya habari vinachangia kumaliza sekta ya muziki wa vijana kwa ajili ya ushindani wa kisifa na biashara unao endelezwa na watu walio waajiri kama presenters wanao rudi nje na kuwa ma meneja na ma promota wa wasanii. Kiwango kikubwa cha wasanii ni masikini sababu ya ushindani na ufisadi katika sekta hiyo vile vile. Wakiniona nafanya kitu hawataki nipate sifa hiyo watanizibia nisionekane kisha waibe wazo langu na kuliwakilisha kwa waajiri wao kama wazo lao ili waongezewe mishahara na vyeo makazini na kuniwacha nikiathirika na familia yangu!

Tunashindana kidini na tunashindana ki siasa badala ya kushirikiana kwa umoja. Jambo hilo limefanya kuelekea kushindana ki kabila. Ni aibu sana watu wazima wanapo jigamba kuwa wasomi lakini ni wakabila na wafisadi ndani ya nafsi zao maana ni watu washindani wasio kubali kushindwa. Kiongozi mzima anashindana na mwenzie eti yeye ametahiri na jamii nyingine haija tahiri kwa hiyo hawastahili uongozi? Huo ni ushindani wa kipumbavu kabisa. Makanisa nayo yanashindana, dini zenyewe ziko na madhehebu yanayo shindana, ndani ya makabila pia kuna mashindano ya ki ukoo!!! Uchawi, uizi na ubedui yote yanaletwa na ushindani katika jamii.

Upendo ni jambo lenye thamani kubwa sana na la ajabu ni kwamba kumpa mtu upendo haigharimu lolote. Ni jambo la bure kabisa maishani. Lazima tufundishane upendo na ushirikiano kuanzia majumbani mwetu na mashuleni ili tuangamize ufisadi. Kila jambo zuri huanzia na mtu mwenyewe kubadili mawazo yake yaliyo muelekeza kufika katika hali mbaya aliyoko kwa sasa. Tukikosa kulipatia jambo hili kipa umbele na kuzidi kuendeleza ushindani maishani, basi mwishowe hakutakuwa na mshindi yeyote. Sote tutaishia kuwa washindwa maana siku moja walio chini watakosa subira na kuamua kuteka kwa nguvu heshima na hadhi ya jamiii kupitia ufisadi na ukatili utakao walenga wale wanao onekana kuwa na hali nzuri ya maisha. Ni bora tufutilie mbali ushindani katika siasa pia, na tuhubiri siasa za ushirikiano na upendo katika jamii zetu ili sote tuje kufaulu. Makabila yote yanapaswa kushirikiana kwa umoja ili Kenya iende mbele. Nawasihi viongozi wasinipuuze na wanisikize.

HATUWEZI KUMALIZA UFISADI NA KUELEKEA KUWA NA UMOJA WA AFRICA MASHARIKI AMA AFRICA NZIMA HADI TUTAKAPO MALIZA USHINDANI WA KISIASA KATIKA NCHI ZETU NA KUHUBIRI USHIRIKIANO WA KISIASA NA UMOJA WA MAKABILA YOTE!