SAFISHA ROHO….USIOGOPE AIBU!!

Posted on

Namshukuru mwenyezi Mungu sana kwa kunipatia huu UFUNUO. Mara nyingi mimi hukuta kwamba jambo ambalo rahisi kumuumiza mtu sana kifikra na ki mawazo, kwangu huwa sio la kunikera mno. Si sengenyi mtu kwa hiyo siogopi kusengenywa. Nikiwa na kero lolote lile mimi nalitoa moyoni. Maisha ni mara moja sitaishi mara mbili. Bora niwe na Uhuru wa kwenye nafsi yangu kuliko kitu chochote kile. Kama nime wahi kutenda kosa au kuchukuwa hatua mbaya ya ki maisha itakuwa ni vibaya sana kwangu kuligeuza kosa lile na kuwa siri eti naogopa aibu, kwa sababu nime wahi kuathirika kwa kutokubali makosa yangu na kuendelea kuficha aibu!

Ninavyo jihisi najua mimi mwenyewe…Uwezo wangu humu duniani vile vile naujua mimi mwenyewe na hakuna yeyote yule anaweza kusema ya kwamba ananifahamu mimi….HAKUNA. Na vile vile wewe unajijua mwenyewe na hakuna yeyote yule anaweza kukujua zaidi yako na ndiyo maana sipendi kusikiza wa mbeya na wasengenyaji. Siko duniani kuchunguza maisha ya mtu bali niko humu duniani kutimiza yale ambayo Mola wangu alinituma ni timize na ni wazi ya kwamba mimi ni mwalimu katika jamii. Nafunza kulingana na niliyo yaona na yale niliyo yapitia mwenyewe maana niko na kizazi nyuma yangu

Nampenda sana mke wangu na watoto wangu japo nimepitia naye majaribio mengi sana nao. Ukweli ni kwamba sote ni wanafunzi katika maisha na tunaenda tuki jifunza. Jambo la muhimu duniani ni kuvumiliana na kuheshhimiana. Muhimu kabisa ni kutakiana mazuri na kuombeana mema.

Hakuna kitu kinaweza kulinganishwa na Nasfi iliyo huru na kuridhika bila siri, uhasama, udhaifu, unyonge ama lawama. Japo binadamu wa leo fikra zake zimekuwa hafifu sana za kutegemea vyombo vya habari kama mwongozo wa gumzo zao vikaoni. Nimekataa kuwa AVERAGE katika gumzo zangu. Nimekataa kuwa AVERAGE kimawazo na fikra. Nimekataa matendo AVERAGE ya kila siku eti ndiyo niingie katika PEER groups na ku fit kwa society…Bora nipate ma fans kutokana na ukweli ninao usema na kuzisafisha nafsi za waathirika wenzangu na wala sihitaji sana marafiki wanafiki.

Mazingira yako ni muhimu sana katika kuyatimiza mafanikio yako ya kuwa humu duniani. Sija wahi mwenyewe kuamini kuwa nilikuja humu duniani nipate mali nyingi kisha nife niwache urithi kibao….Hapana… nahisi nililetwa humu Duniani kutimiza jambo flani SPECIAL maana mimi mwenyewe special kichizi ndo maana Mungu akanikubalisha nizaliwe na niishi hadi kuiona siku hii ya leo niweze kuandika kitu special kama hiki kitakacho wafanya wale special wengine nao waamke kufanya juhudi za kutimiza maono yao.

2 thoughts on “SAFISHA ROHO….USIOGOPE AIBU!!

  1. R.I.C Baraka zikufuate tele, nimezoa maneno ya muhimu kutoka kwako.

    1. asante sana Brian nimeshukuru support yako bro. Barikiwa sana kaka.

Comments are closed.