HAMNA KITU KAMA “ZARE”, CHUKUA HATUA

Posted on

Ukweli ni kwamba wengi wetu tupo na ndoto na maono kubwa kubwa ndani zetu katika kutenda mambo flani yaliyo na manufaa tele katika jamii na kwa wanadamu kwa ujumla, na ndiposa baadhi zetu tupo mbioni kuzitimiza. Unapo aminia yale maono uliyo nayo huwa inakuwa jambo zuri sana na hatimaye huwafanya watu walio kuzunguka pia kuamini ya kwamba unao uwezo wa kutimiza maono yako na ndiposa hao huamua kujiunga na wewe wakusaidie ili utimize ndoto hizo.

Nadhani ya kwamba wanariadha wetu wa kenya ni mfano mzuri kabisa. Hao huweka wakati mwingi sana katika mazoezi na maandalizi na hupitia mitihani mengi kabla serikali na mashirika mengine ya ki biashara kuamua kuwapa support ya kifedha wanariadha hao na pia kupewa hadhi kuu na serikali kuwakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya riadha pande tofauti ulimwenguni.

Sasa basi ukija katika usanii hamna tofauti yoyote, msanii unapaswa kuaminia maono yako na uchukuwe hatua kuyafikia malengo yako. Hakuna kitu kama ONE DAY NITA MAKE IT….. Amka na kisha chukua hatua itakayo kufikisha katika malengo yako. Usingoje zare…mtu wa kungoja zare huwa ndiye rahisi kabisa kuwa snitch katika game hii. Ukitaka ku make it basi una have ku CREATE IT……Amka u create vile Uta make!!!
Kama inabidi usome ndiyo uweze kufahamu mambo flani yatakayo kusaidia uyafikie malengo yako basi unangoja nini? Get Up and learn something!!! AMKA UJIFUNZE KITU…haina aja ushinde kibarazani ama studio uki snitch!

Makosa makubwa tuliyo nayo ni kukataa kuchukuwa hatua ya kutufikisha penye malengo yetu na badala yake tuna aamua bora kulaumu, Mara tunalaumu serikali, mara tunalaumu ma promoter, tunalaumu mashirika na kadhalika…Ukweli ni kuwa hao wote hawana lawama zozote maana ndoto ni zetu, na wala sio zao kwa hiyo hawana lazima sana ya wao kujihusisha na ndoto hizo! Kama tunataka kweli wajihusishe na ndoto zetu basi inabidi tuwape sababu kubwa sana kama vile wanavyo fanya wanariadha ndiposa serikali iwape support, na kumbuka watu ni wengi uwanjani. Inabidi uweke wakati mwingi kwenye maandalizi na mazoezi ili uwe Guru upande wako. Kwa mfano mwana muziki KRS – ONE ni mtu aliye jisomesha mwenyewe hata licha ya kuwa hakuwa na makao maalum kama watoto wenzake. Alijifunza kupitia public libray ya Marekani Bronx ili aweze kufunguka akili na kuwa mwana filosofia mkongwe wa HipHop. Hivi sasa ameandika vitabu vingi licha ya kuwa hakuenda shule. Alichukuwa jukumu la kujifunza na akafaulu.

Acha kuona haya ya kuchukuwa hatua flani maishani ya kubadili mienendo ambayo imekuweka katika suhemu flani ya kimaisha kwa mda mrefu bila mabadiliko. Kama ni kuwacha uraibu mbaya acha, kama ni kujitoa miongoni mwa vikundi potofu jitoe ili mambo yako yawe freshi. Wewe ni champion hata kabla uambiwe na mtu mwingine ya kuwa wewe ni champion. Ulikuwa champion tangu ushinde wenzako zaidi ya millioni tano tumboni mwa mamako na ukadaka yai kwanza, kisha kupitia miezi tisa ya muundo msingi wa mwanadamu uliketi tumboni hadi kuzaliwa. Kila mmoja wetu ni champion na kinacho tutofautisha ni mwenye kuchukuwa hatua na mwenye kuogopa kuchukua hatua ili kuyafikia malengo yako.

Tulipokuwa wadogo tulikuwa na mchezo wa kuruka kamba. Katika huo mchezo mtu huingia tu, na kuanza kuruka. Kila wakati hiyo huwa ni bahati na sibu maana unaweza ukaingia tu na kamba ikakugusa au ukaingia na wala isikuguse ukaendelea kuruka vyema hadi kuchoka. Lakina kuna wale wenzetu walikuwa waoga waliotazamia ile kamba kwa mda mrefu eti waki ngojea wakati mwafaka ndiyo waingie na baada ya mda wao waligundua kwamba wakati umepita mwingi na bado kamba inaenda kwa kasi vile vile na wala hamna mabadiliko…… wengi wetu wamezubaa katika hali ya kungojea kamba ipumzishe makali lakini ukweli ni kwamba wewe ndiye unayepaswa kuchukua hatua kwanza alaf mengine baadaye.
Muwe na Easter Njema.