BUDA BILA KIBOKO….WATAPOTEA!

Posted on

Wana semaga ya kwamba, mtu mbaya kuliko yeyote maishani ni anaye ona makosa yakitendeka na kisha ana puuzilia mbali kwa kugeuza sura upande mwingine na kutazama maonevu au ufukura unapoendelea wakati yeye yuko katika hali ama hadhi ambayo inaweza kuchangia mabadiliko na kuleta hali nzuri kwa watu hao. Acha niwape dili freshi ma dogo wenu wasije wa shangaa mlingoja ku sign dili hadi kufikia umri wa ku retire.

Hii ni kwa wale walioko vitongojini na wanazengulika na picha za kwenye fb, filamu, youtube na kutaka kuwa vile wanavyo onyeshwa bila kujipatia mafunzo flani ya kuwaezesha kujitegemea. Mkwanja ukija kidogo tu unakimbilia kutimiza fantasy na unajaribu kuikwepa reality!!! Ata ni bora uwe rapper na umejifunza guiter au drum kuliko uwe rapper tu unasubiri dili au media ikukubali ndiyo uishi freshi.

Acha upuzi mwanangu na tena zidi kunichukia…buda bila kiboko watoto watapotea na ni desturi zetu waAfrica. Ukipata pesa kwa show usikimbilie pira, pamba, buti ama swagg kwanza au urukie poko flani litakupa ngoma mwanangu na vile ulinicheka itakuwa sasa ni chance yako….UTAPATA NGOMA NA SIO UTANI….huko unaelekea ndiko nitokako ndugu amavipi?
Mda huu tulioko sasa kitu cha busara tena poa ni ku ekeza fedha kwenye rasilimali iliyoko ndani yako. Rasilimali ambayo itakusaidia wewe hata ukifilisika ki muziki bado utaweza kupata afueni na kujistiri kwa njia ya halali. Unaweza kuekeza katika kujifunza lugha flani ya Kigeni, Unaweza kuekeza katika mazoezi ya ki mwili, unaweza kuekeza katika kujifunza jinsi ya kufanya biashara katika social media ama kupata mafunzo kama kutengeneza websites, utendaji biashara za kilimo na kadhalika.

Tukiwa na masela wa hiphop wa kweli walio ni wasanii na vile vile wanasheria, wengine ni wasanii na pia wamesomea mauzo, wengine wamesaomea tarakilishi, wengine wamesomea hata lugha ya Kiswahili, wengine waalimu, wengine ma fitness instrutors, ma graphic designer, ma video producer, ma actor na kadhalika kisha pia umoja uwe kati yetu itakuwa rahisi kujiunga pamoja na kufanya mambo kuliko sote tusibiri AIRPLAY ama TV INTERVIEWS ndiyo tunufaike na sanaa yetu. Ukweli ni kwamba upo upungufu katika nyanja tofauti kutokana na wasanii wengi kupuuzilia mafunzo na kutegemea rhymes peke yake.

Nafasi ni kibao, na mda unao kibao. Usipoteze mda nanii, changamka na uchukuwe hatua ya kujiendeleza kimaisha acha propaganda na siasa za peni mbili kwenye industry. Watu wanataka ajira na kuna vile munaweza kujitengenezea ajira kibao sana bora mchukue huo uamuzi ndo tusaidiane. Sio lazima sote tuwe ma rapper na ma producer. Hata ndiyo maana ma producer wetu wa hiphop wengi ni mwani hata masela marappa bado wengi mwani. Kitu bora sasa hivi ni wengine nao wajifunze mambo mengine hata sheria na mauzo, na kadhalika, ili ndiyo ule msemo wa “sisi kwa sisi” uwe ni wa kweli katika ku enuana na ku endelezana ki maisha wala sio wa ku baguana na ku tengana kisifa. Tuko pamoja kama kawaida hapa kwangu mambo barida!